Monday, 16 November 2015

BREAKING NEWSSSSS .......CCM YAMTEUA NDUGAI KUWANIA USPIKA, RAIS MAGUFULI AMTEUA DK. TULIA KUWA MBUNGE


RAIS Dk. John Magufuli amemteua Dk. Tulia Akson kuwa mbunge wa kuteuliwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk. Tulia amekuwa mbunge wa kwanza wa kuteuliwa na Rais Magufuli tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wadhifa alioteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Septemba, mwaka huu.

Awali, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM walioomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge. Wengine ni Naibu Spika aliyemaliza muda wake, Job Ndugai na Abdulla Mwinyi.

Hata hivyo, habari zilizopatikana hivi punde zimeeleza kuwa, Dk. Tulia na Mwinyi wamejitoa katika kuwania nafasi ya kuwania Uspika na kumwacha Ndugai awe mgombea pekee.

Kutokana na uamuzi huo wa Dk. Tulia na Mwinyi, Ndugai anakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo. Uchaguzi wa Spika wa Bunge utafanyika kesho.

Aidha, upo uwezekano mkubwa wa Dk. Tulia, ambaye ameteuliwa kuwa mbunge, akachaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge.

No comments:

Post a Comment