RAIS Dk. John Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade.
Kusimamishwa kwa Bade kumekuja muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kutembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TRA) na kuibua madudu ya kiutendaji ndani ya mamlaka hiyo.
Sambamba na hilo, Rais Dk. Magufuli amemteua Dk. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo Dk. Mpango alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango na amemtaka Bade kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Mapema akiwa katika bandari ya Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Tiagi Masamaki, na watumishi wengine wanne kutokana na upotevu makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80.
Wengine ni Habibu Mponezya wa kitengo cha huduma kwa wateja, Haruni Mpande wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT0, Hamis Omari na Eliachi Mrema ambaye ni msimamizi wa Bandari Kavu (ICD), ambayo ilihusika na upotevu wa makontena hayo.
Majaliwa alisema serikali haiwezi kuvumilia kuona mapato yanapotea huku watu waliopewa dhamana ya kusimamia wakishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru.
Ziara ya Majaliwa ililenga kuangalia namna shughuli zinavyoendelea katika bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.
Alisema alitaka kujua kwa nini mfanyabiashara achukue mizigo yake bila kulipia ushuru na kutaka kupatiwa maelezo ya kuwepo kwa sekeseke la kupotea kwa makontena 349.
Bade alisema tayari suala hilo wanalifanyia kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na walishaenda kwenye ICD iliyohusika na upotevu huo ambayo alisema imeshafunguwa.
Majaliwa alihoji umakini wa TRA wa kuendelea na uchunguzi dhidi ya jambo hilo wakati wahusika wakiwemo wengine kama Mponezya wakihamishwa.
“Kama mko makini wafuatao wasiendelee kuwepo kazini. Naanza kwa Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki. IGP amkamate na anyang’anywe hati ya kusafiria ili akasaidiane na polisi katika uchunguzi wa tukio hili.
“Habibu Mponezya naye akamatwe na hati yake ya kusafiria ikamatwe, mali zake zifanyiwe uchunguzi ili kuangalia kama zinaendana na kiwango cha utumishi wake na kitengo cha ICT kidhibitiwe kuanzia sasa,” alisisitiza Majaliwa.
Mbali na kumwagiza IGP kuwakamata vigogo hao, pia aliuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kuwahamishia mikoani watumishi watatu ambao ni Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandegele na Robert Nyoni.
Majaliwa ambaye alitinga bandarini hapo akiwa na orodha ya namba za makontena yaliyopotea katika karatasi kubwa, alisema serikali imejipanga kuwashughulikia watu wajanja wajanja ndani ya TRA.
Alisema anahitaji kupelekewa jina la mfanyabiashara mwenye mzigo huo na pia lazima TRA imchukulie hatua kabla ya wao kufanya uamuzi lazima walinzi nao waondolewe kwa sababu anafahamu kuwa mizigo yote imepitia katika geti namba tano.
Pia Majaliwa alimtaka Bade amweleze maeneo ambayo yanampa shida katika kutambua mianya ya wizi. Bade alisema ni pale ambapo mizigo inaelezwa kuwa ni ya kwenda nje kumbe inatumika ndani.
Katika hatua nyingine, Majaliwa alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, DK. Likwelile, apeleke watu wa serikali mtandao (e-government) ili wafanye uchunguzi na kubaini njia zote yalikopita makontena hayo hadi ICD.
Alisema anahitaji kufahamu mizigo iliyokuwemo na kama ingelipiwa kodi zingepatikana sh. ngapi na kuwataka makatibu wakuu wa wizara za Uchukuzi, TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Fedha kuweka mikakati itakayowezesha kupatikana kwa fedha hizo.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amesema serikali ina orodha ya wafanyabiashara 300 waliopitisha makontena yao bandarini bila kulipa kodi.
Pia amesema wafanyabiashara wote wenye madeni ya kodi na baada ya muda wakatangaza kufilisika kwa kampuni zao, watambue kuwa madeni hayafilisiki na wanatakiwa walipe.
Balozi alitoa taarifa hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Ikulu jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Majaliwa kufanya ziara bandarini.
Alisema wana orodha ya wafanyabiashara wote kwa kuwa wamefanya uchunguzi wa muda mrefu na wanajua kila kitu, hivyo wanawaomba wafanyabiashara waliotoa makontena yao na hawakulipa ushuru waende wakalipe.
“Waende wakalipe fedha zao. Tutakapoanza hakutakuwa na msamalie mtume kwa kuwa tumejiandaa vya kutosha kuhakikisha tatizo hili la ukwepaji kodi linakwisha kabisa,” alisema.
Hivyo, alisema kazi ndio kwanza imeanza hivyo wale wafanyabiashara waliofunga kampuni zao na kutangaza zimefilisika walipe madeni yao kwa kuwa madeni hayafi.

No comments:
Post a Comment