KASI ya utendaji ya Rais Dk. John Magufuli, imewazindua viongozi wa kada mbalimbali na sasa wameanza kuchukua hatua kadhaa katika kutekeleza majukumu yao.
Viongozi ambao wameonekana kuzinduka na kuanza kuendana na kasi hiyo ni makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa mikoa na wa wilaya ambao kama ilivyo kwa Rais, wameanza kufanya ziara za kushitukiza katika maeneo yao ya utawala na hata kutoa maagizo mazito kwa watu wa chini yao.
Katika kundi hilo, pia wamo vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wameanza kuchukua hatua kadhaa dhidi ya watu wanaokwepa kulipa kodi huku wakionya kuwa hawatakuwa na msalia mtume dhidi ya watu hao, hususan wafanyabiashara.
Wiki hii, mathalan, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipakodi wa TRA Richard Kayombo, alisema wameanzisha operesheni katika bandari kazi nchini kwa lengo la kubaini kama kodi zinalipwa ipasavyo.
Alisema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha kila mtu analipa kodi inavyostahili na kwamba
mamlaka hiyo haitamwonea haya mfanyabiashara yeyote atakayekwepa kodi.
Sambamba na kutoa maagizo hayo, uchunguzi uliofanywa na Uhuru Wikiendi unaonyesha kwamba baadhi ya vigogo hao wameamuru baadhi ya watumishi wasiofuata maadili ya kazi zao kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Kadhalika, habari zaidi ambazo Uhuru Wikiendi imezipata zinasema hata badhi ya vifaa ambavyo vilikuwa vimewekwe kwenye ofisi za wizara na idara husika mikoani, ambavyo vilikuwa vikibanwa makao makuu ya wizara au taasisi, vimeanza kupelekwa.
Kabla ya Rais Dk. Magufuli kuingia madarakani, baadhi ya watendaji makao makuu ya wizara mbalimbali walikuwa hawatoi vifaa kwa idara na ofisi zilizoko mikoani huku wakijitetea kuwa fedha kwa ajili ya ununuzi wa zana hizo hazijatolewa.
Lakini sasa vifaa hivyo vimeanza kupelekwa hivyo kuwashangaza baadhi ya watendaji na kuona ni kama muujiza.
SADIKI ACHARUKA
Katika kutekeleza agizo la Rais Dk. Magufuli juu ya kuitumia Desemba 9 kufanya usafiikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema wamejipanga kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kikamilifu.
Akizungumza na vyombo vya habari juzi, Sadiki alisema agizo la Rais litakuwa mwanzo wa kuliweka jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafina kupambana na magonjwa ya mlipuko, kikiwemo kipindupindu.
Alisema mkoa unajipanga kuhakikisha kuwa suala la usafilinakuwa la lazima katika maeneo yote na kila mtu ni lazima ashiriki kikamilifu. Kwa kufanyahivyo, alisema majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakiuandama mkoa yakiwemo mafuriko, itakuwa historia.
Kwa mujibu wa Sadiki, hatua hiyo pia itapunguza hata fedha za serikali ambazo zimekuwa zikitumika katika majanga mbalimbali. Alitoa mfano wa kipindupindu ambacho kilijikita mkoani mwake na kusababisha sh. bilioni 1.8 kutumika kukidhibiti.
Wakati Sadiki akisisitiza hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, alitembelea Kata ya Wazo, Manispaa ya Kinondoni ili kujionea hali halisi ya migogoro ya ardhi.
Kutokana na ziara yake hiyo, Makonda alisema zaidi ya ekari 26,000 za ardhi wilayani humo zitahakikiwa kutokana na kuwa katika migogoro ya muda mrefu.
Kabla ya viongozi hao kufanya hivyo, katika manispaa zote tatu za jiji laDar es Salaam, iliendeshwa bomoabomoa katika maeneo ambayo ujenzi wake ulikiuka sheria za mipango miji. Katika bomoa bomoa hiyo,baadhi ya majumba ya kifahari yalivunjwa.
MONGELLA AIBUKA
Mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa, John Mongella, amesema wataitumia Desemba 9 kuwa siku ya usafikama alivyoagiza Rais Dk. Magufuli ikiwa moja ya jitihada za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Mongella alizindua jana Operesheni Tokomeza Kipindupindu Kagera, ambapo alimwagiza Ofisa Afya wa Manispaa ya Bukoba, Ladislaus Oisso, kufunga migahawa na vilabu vya pombe za kienyeji ambapo mazingira yake yameonekana yakiwa katika hali ya uchafu.
Maeneo yaliyohusika na operesheni hiyo ambayo mkuu huyo alitembea kwa miguu huku akishirikiana na wanachi kufanya usafini Kata za Bakoba, Kashai, Miembeni na Bilele.
Aliwaagiza maofisa wa afya afya kuzibua mitaro, kuondoa na kuoza taka ngumu zilizoko katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Aidha, Mongella aliagiza kuwa ifi kapo Jumanne ijayo, ugonjwa huo uwe umekwisha kabisa katika maeneo yote ya mkoa na endapo katika nyumba fulani atapatikana mgonjwa wa kipindupindu, hatua stahili zitachukuliwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson Msome, alisema serikali imeshtushwa na ongezeko la haraka la wagonjwa 10 ndani ya saa 24 ambapo Novemba 22, mwaka huu, walikuwa 16 lakini baada ya siku mbili waliongezeka hadi 26.
MAKALA AZIONYA SHULE
Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala amezionya bodi za shule ambazo zimekuwa zikipandisha michango bila kuwa na sababu za msingi na kutoishirikisha serikali.
Makala alitoa kauli hiyo jana alipofanya kikao cha kupeana majukumu, ambacho kiliwakutanisha wakuu wa wilaya zote za mkoa, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara mbalimbali katika kila halmashauri.
Alisema kuna baadhi ya bodi za shule zimekuwa zikipandisha michango mbalimbali na isiyo ya lazima ambapo wanafunzi wamekuwa wakichangishwa sh. 50,000 kila mmoja na zingine zaidi ya kiwango hicho. Aliagiza kwamba michango yote hiyo inapasa kuondolewa.
“Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi mnapaswa kutekeleza agizo la Rais, kwa kutoa Elimu bure. Hii nataka kuona linatekelezeka kwa ufasaha zaidim,îalisema.
Makala alisema kwa sasa wanasubiri utaratibu kutoka TAMISEMI kujua mfumo wa utozwaji wa michango mingine utakuwaje, ili kuhakikisha michango itakayotozwa na shule zilizoko mkoani Kilimanjaro inalingana na michango ya shule zilizoko katika mikoa mingine.
Katika hatua nyingine, Makala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi, kuanzisha operesheni kali kwa ajili ya kutokomeza dawa za kulevya aina ya mirungi. Wilaya hiyo inaongoza kwa uzalishaji wa mirungi.
Makala alisema katika kuhakikisha agizo la Rais Dk. Magufuli la kupiga vita biashara ya dawa za kulevya, ni lazima kila mtumishi wa serikali kuwajibika katika kutekeleza agizo hilo.
Alisema wilaya ya Same ni miongoni mwa wilaya ambazo zimekidhiri kwa biashara ya mirungi pamoja na kilimo cha mmea huo, ambapo wafanyabiashara wengi wanaokamatwa hudai wanatoa Same.
“Ili kuhakikisha kuwa biashara ya dawa za kulevya inakoma katika nchi yetu, ni lazima kwanza kuhakikisha tunapadhibiti pale kwenye chanzo.
Nawapongeza sana wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA), kwa kudhibiti ipasavyo. Sasa nataka na mkuu wa wilaya ya Same ukitoka hapa nenda kaanzishe operesheni kali ili kuwakamata wale wote wahusika pamoja na kutafuta mashamba yaoî alisema.
Makala pia aliwataka watumishi wote wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Alisema baadhi yao wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mambo yao ikiwemo kuchati katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, alitangaza kufutwa kwa ruhusa na likizo kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na maofisa waandamizi wa serikali mkoani humo katika kipindi cha Desemba kwa kile alichosema ni kutaka mkoa kuendana na falsafa ya “Hapa Kazi Tu”.
GALAWA AJIPANGA
Katika kutekeleza agizo la Rais Dk. Magufuli, la kufanya usafiDesemba 9, mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, ashakutana na viongozimbalimbali wa mkoa na taasisi zilizoko mkoani humo kujadili na kupanga mikakati.
Vile vile, Chiku amekutana na maofisa watendaji wa kata na maofisa maendeleo ya jamii, afya, usafina mazingira na waratibu elimu kata na kupanga namna bora ya utekelezaji wa agizo hilo.
Katika uamuzi uliofikiwa, uongozi wa mkoa umepanga kazi hiyo kufanyika kabla ya siku iliyopangwa na kwamba itakuwa endelevu na kwamba itafanyika kuanzia saa moja hadi saa tatu asubuhi.
MA-DC NAO WAWA MBOGO
Katika kuonyesha kuwa hakuna mzaha kwenye utekelezaji wa maagizo ya Rais, likiwemo la kufanya usafiDesemba 9, baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa mbogo na kutaka wananchi watekeleza na kutimiza wajibu wao.
Mbali na utekelezaji wa usafi, wakuu hao pia wameanza kufuatilia matukio kadhaa anayofanywa kwenye maeneo yao ya utawala na kuchukua hatua mbalimbali.
Wilayani Bunda, Mara, Mkuu wa Wilaya hiyo, Joshua Mirumbe, ameagiza mfamasia wa Hospitali Teule ya Wilaya, Clyvanus Katula, kuchukuliwa hatua za nidhamu baada ya kuwanyima dawa wagonjwa.
Mfamasia huyo alikataa kutoa dawa kwa wananchi wawili wanatumia dawa za kurefusha maisha (ARV) baada ya kwenda kuzifuata katika hospitali hiyo.
Katula anadaiwa kuwafokea wananchi hao kuwa waondoke na ndipo walipochukua hatua za kulifikisha suala hilo katika ngazi husika.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, kumsimamisha kazi mara moja muuguzi wa zahanati ya Kambarage, anayetuhumiwa kuiba dawa.
No comments:
Post a Comment