NA REHEMA SHABAN, TSJ
SERIKALI imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekomba fedha Hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Pia imewataka wananchi wapuuze habari hiyo kwa kuwa hazina ukweli wowote.
Kamishna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, John Cheyo, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi la Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.
“Hazina inazo pesa za kutosha na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu, kununua mashine za BVR kwa kutumia pesa za Watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu,” alisema.
Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea kusema mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 ni sh. trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

No comments:
Post a Comment