WAFANYAKAZI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), wametakiwa kurudisha posho walizopewa kwa ajili ya safari ya kwenda katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Kila Desemba Mosi, huadhimishwa Siku ya Ukimwi Duniani na mwaka huu sherehe hizo zilipangwa kufanyika mkoani Singida.
Hata hivyo, Rais Dk. John Magufuli, alitangaza kufuta maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikiwa sehemu ya mkakati wa serikali yake wa kufuta matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.
Kutokana na kufutwa kwa maadhimisho hayo, wafanyakazi wa tume hiyo, waliokuwa wamepewa za safari na kujikimu kwa ajili ya shughuli hiyo, wametakiwa warejeshe.
Pia waliokwenda mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho hayo, wametakiwa kurudi mara moja katika vituo vya vya kazi.
Habari za kuaminika zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam, zilidai kuwa baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo walikuwa mkoani humo, kabla ya Rais Dk. John Magufuli, kuyafuta maadhimisho hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alidai kuwa wale walioko mkoani humo wanatakiwa kurudi mara moja ila kwa wale ambao walishapewa fedha na walitarajiwa kuondoka hivi karibuni, wameandikiwa barua za kurejesha fedha hizo.
“Bora Rais Dk. John Magufuli amesimamisha maadhimisho hayo ambayo yalijaa upendeleo wa hali ya juu, maana kila mwaka wanaenda wale wale na kujipatia fedha nyingi na sisi tunabaki kulinda ofisi.
“Alivyofanya Rais anastahili pongezi kubwa. Huo ni ubadhirifu wa fedha na wanalipana posho kubwa mno bila ya sababu za msingi,” alisema mfanyakazi huyo.
Habari hizo zilidai kuwa wafanyakazi waliochukua fedha hizo wameanza kuhaha kwa kuwa baadhi yao walishazitumia kwa matumizi hayo ya maandalizi ya safari.
Alisema serikali imefanya jambo la maana kusimamisha maadhimisho hayo, kwanza hayasaidii chochote watu wanakufa kwa kukosa dawa bora hizo fedha zikanunue dawa.
“Ukienda hospitalini kwa kweli inatia huruma hasa vijijini watu wengine wakienda hospitali hawapati dawa na wengine inawalazimu kwenda maeneo mengine kufuata,” alisema.
Mfanyakazi mwingine wa taasisi hiyo, ambaye naye hakutaka kutaja jina lake, alimpongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake wa busara wa kusitisha maadhimisho hayo.
Alidai maadhimisho hayo yalikuwa yakitumia fedha nyingi za serikali, badala ya kununulia dawa na kuboresha vituo vya afya vinavyotoa dawa za kurefusha maisha.
Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo, mianya ya rushwa, ubadhirifu na asilimia 10 waliyopata katika kuandaa sherehe yoyote katika kuwalipa wapambaji na wale wanaotengeneza chakula kwa ajili ya wageni.
Hata hivyo, Uhuru Wikiendi ilimtafuta Ofisa Habari wa TACAIDS, Nadhifa Omary, bila mafanikio kwa kuwa simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila majibu.
Juzi, Rais Dk. Magufuli alitangaza kusimamisha maadhimisho hayo na badala yake fedha zilizopangwa kutumika katika sherehe hizo, kuelekezwa kwenye matumizi mengine ikiwemo ununuzi wa dawa za ARV.

No comments:
Post a Comment