Thursday, 31 December 2015

SERIKALI YATOA BILIONI 18.77 KUGHARAMIA ELIMU BURE SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI



NA THEODOS MGOMBA, DODOMA

SERIKALI imetoa sh. bilioni 18.77 , ikiwa ni fedha  kwa ajili ya kugharamia utoaji elimu bure kwa shule za msingi na sekondari kuanzia mwakani.

Fedha hizo zitatolewa kila mwezi. Imeelezwa kuwa fedha hizo zitapalekwa moja kwa moja kwenye shule husika baada ya kutolewa na Hazina.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais (TAMISEMI), George Simabchawene,  alisema fedha hizo zitatumika kwa ruzuku ya uendeshaji shule. Kwa upande wa chakula alisema serikali imetoa sh. 1,500 kwa siku kwa kila mwanafusi  wa shule ya msingi na sekondari anayekaa  bweni.

Kwa mujibu wa Simbachawene, fi dia ya ada ya sh. 20,000 imetolewa na serikali kwa mwanafunzi wa kutwa na sh. 70,000 kwa wale wa bweni. Alisema kuanzia mwakani, gharama za mitihani ya kidato cha nne zitalipwa moja kwa moja kwa Baraza la Mitihani la Taifa.

“Hivyo kuanzia mwakani wazazi au walezi hawatatakiwa kulipa gharama hizi, tutatumia fedha hizo hizo za mafi sadi kuwalipia watoto wetu gharama hizo,’’ alisema. Waziri Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi kuhakikisha utekelezaji wa elimu ya msingi bila malipo unafi kiwa.

Alisema kiongozi yeyote ambaye atabainika kwa namna moja au nyingine kutofanikisha suala hilo atachukuliwa hatua kali.

“Ikumbukwe kuwa tumejiwekea malengo ya kuinua kiwango cha ufaulu kupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), hivyo kila mhusika atimize wajibu wake,” alisema.

Alisema mikoa ambayo haikufanya vizuri katika ufaulu mwaka huu, wahusika wote watoe maelezo ni kwanini hawakufi kia malengo.

Aidha, aliwataka wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kuhakikisha kuwa ifi kapo  Februari 15, mwakani, wawe wamekamilisha miundombinu ya shule, ili vijana 12,647 ambao walikosa nafasi waweze kuingia shule.

Katika hatua nyingine, Simbachawene amewasimamisha kazi maofi sa biashara wawili wa Manispaa ya Dodoma kwa urasimu na kusababishia manispaa hiyo kupata hasara ya sh. milioni 75.

Akitoa taarifa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TAMISEMI, Rebecca Kwandu, alisema watumishi hao walisimishwa kazi kuanzia jana. Rebecca alisema Waziri Simbachawene aliwasimamisha  kazi aliyekuwa Kaimu Ofi sa Biashara, Elias Kamara na msaidizi wake Donatila Vedasto.

Alisema  Simbachawene alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwaondoa kazini watumishi hao na nafasi zao kujazwa na watu wengine. Alisema katika uchunguzi uliofanyika baada ya malalamiko ya watu, ulibaini kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu ya msingi.

“Kutokana na hali hiyo ya kukalia maombi hayo bila sababu, manispaa hiyo imekosa kiasi cha sh. milioni 75,’’ alisema Simbachawene.

Alisema kukaliwa kwa maombi hayo bila sababu kunaashiria vitendo vya rushwa. Waziri huyo aligiza maofi sa wote wa biashara nchini kuhakikisha kuwa watu wanaoomba leseni kuanzia sasa wapewe katika kipindi cha siku mbili hadi tatu tu.

“Sitaki urasimu katika utoaji wa leseni, kwani hakuna sababu ya mtu kusubiri kwa muda mrefu kitu ambacho kinaweza kupatikana kwa muda mfupi,’’alisema.

Aidha, alisema ofisa biashara yeyote atakayebainika kufanya urasimu adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.

CHANZO CHA HABARI: GAZETI LA UHURU

No comments:

Post a Comment