Thursday 7 January 2016

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WATOTO WA KUBAMBIKIWA




MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyelle, ametoa ufafanuzi wa taarifa zinazohusu asilimia 47 ya watoto wanaozaliwa hapa nchini kuwa si wa baba husika.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, juzi, Profesa Manyelle alisema, vyombo vya habari vilimnukuu vibaya kwa vile asilimia hiyo ni ile ya maombi yanayowasilishwa ofisini kwake, sio nchi mzima.
Alisema asilimia 47 ya maombi yanayowasilishwa katika ofisi yake kuchunguzwa, yalionekana kuwa na matokeo hayo, na si kwamba yalihusu nchi nzima.
Profesa Manyelle alitoa ufafanuzi huo, baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, kumuuliza kuhusu ukweli wa taarifa hizo, huku akitaka kujiridhisha juu ya vipimo vya kutambua vinasaba (DNA), kubaini ukweli juu ya mtoto.
“Tulizungumzia kuhusu sampo zilizowasilishwa ofisini kwangu, ambazo baada ya kuzifanyia uchunguzi, tulibaini matokeo hayo kwamba, asilimia 45  za sampo hizo, watoto walionekana si wa baba husika,” alisema Profesa Manyelle.
Kutokana na ufafanuzi huo, Dk. Kigwangwalla alikanusha taarifa hizo zilizokuwa zimeenea na kwamba ziliwadhalilisha wanawake kwa sababu zilitoa picha tofauti.

No comments:

Post a Comment