Thursday 30 June 2016

POLISI YAUA MAJAMBAZI MATATU MAPANGO YA AMBONI

OPERESHENI Maalumu ya vikosi vya kijeshi imefanikiwa kuwakamata na kuwaua watu watatu ambao wanadaiwa kuhusika na mauji ya watu wanane wa Kitongoji cha Kibatini na matukio  mengine yaliyofanyika jijini Tanga hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Leonard Paul,  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika msiti wa kitongoji cha Kibatini umbali wa kilometa nane kutoka Tanga mjini.

Alisema watu hao waliouawa ni viongozi wa kikundi hicho kilichokuwa kimepiga kambi katika mapango ya amboni .

Aliwataja waliouawa kuwa ni Abdulkadir Singano, Ramadhani Mohamedi na Seifu Jumanne na kwamba uchunguzi umebaini walifanya mauaji na matukio mengine mjini humo.

Kamanda huyo alisema katika oparesheni hiyo walifanikiwa kukamata silaha aina za SMG mbili, bastola moja, risasi 30 za SMG, sufuria, madumu ya maji, nguo, viatu, madumu ya mafuta, mapanga, visu, majambia na vifaa vya kichawi.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni dawa za kienyeji na makopo yenye dawa ambavyo vinavyosadikiwa kuwa ni vya kichawi.

“Mkoa wetu sasa ni salama kabisa hakuna tena uhalifu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejihakikishia kuwa hali ni shwari,”alisema kamanda huyo na kuwa kwa sasa hali ipo shwari na ulinzi umeimarishwa.

No comments:

Post a Comment