Monday 16 January 2017

BULEMBO, KABUDI WATEULIWA KUWA WABUNGE



RAIS Dk. John Magufuli, amefanya uteuzi wa wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na balozi mmoja.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana, ilisema wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Bulembo na Profesa Palamagamba Kabudi.

Ilisema wabunge wateule wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Dk. Magufuli amemteua Benedicto Mashiba kuwa balozi.

"Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Mashiba itatangazwa baadaye," ilisema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment