Wednesday, 4 January 2017

WALIOIBA FEDHA BENKI YA FNB KIZIMBANI


WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kujibu tuhuma za wizi katika benki ya FNB.

Washitakiwa hao ni Noela Kobello (30) na Christopher Delasio (20).

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Doroth Massawe, ulidai mbele ya Hakimu Mkazi, Obadia Bwegege kuwa, washitakiwa walitenda kosa hilo Desemba 17, mwaka jana, katika eneo la Msasani, wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Massawe alidai watuhumiwa walijaribu kuiba fedha katika Benki ya FNB, iliyoko tawi la Msasani, ambapo kabla hawafanya jaribio hilo, walitumia nguvu dhidi ya Grace Sonje, Regina Ngulana na Oscar Mponda ili kupata fedha hizo.

Washitakiwa walikana shitaka hilo, ambapo Noela aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana na Delasio alirudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.

Hakimu Bwegege alitoa masharti ya dhamana yaliyowataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja, watakaotia saini dhamana ya sh. milioni tano.

Kesi hiyo itatajwa tena Januari 16, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment