Friday 10 February 2017

MANJI, GWAJIMA WAENDELEA KUSOTA RUMANDE


Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendeleea kuwashikilia Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji na Askofu Josephat Gwajima kwa zaidi ya saa 24 mpaka sasa.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema kuwa watu hao jana walifika hapo na kukutana na wapelezi .

“Watu hawa wamehojiwa kuanzia jana mpaka saa za usiku kisha wakawekwa mahabusu  hivyo mpaka sasa ninavyozungumza wapo mahabusu wakisubiri utaratibu mwingine” amesema  kamanda Siro.

No comments:

Post a Comment