Wednesday 12 July 2017
BODI YA MIKOPO YAKUSANYA DENI LA BIL. 216.9/-
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema urejeshaji wa mikopo kwa wadaiwa sugu kwa mwaka wa fedha 2016/2017, umewawezesha kukusanya sh.216,992,990,152.98, kati ya 427,708,285,046.48.
Pia, imesema katika fedha hizo, asilimia 65 ya marejesho hayo imetoka kwenye sekta ya umma huku sekta binafsi ikiwa asilimia 35.
Akizungumza jana, Dar es Saalam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razzaq Badru, alisema makusanyo hayo kutoka sekta ya umma yanaonesha kuwa, asilimia tisa zimetoka serikali kuu, ambazo ni zaidi ya sh. 12,694,089,923.95.
Mkurugenzi Mtendaji huyo aliongeza kuwa, asilimia 69 ya makusanyo hayo zilitoka serikali za mitaa, ambazo ni zaidi ya sh.97,321,356,083.61 wakati sh.31,029,997,591.88, sawa na asilimia 22, zilitoka kwenye wakala za serikali na taasisi nyingine.
“Mchanganuo wa mikopo iliyokusanywa kutoka sekta binafsi unaonesha kuwa, makusanyo kutoka sekta ndogo ni shilingi 23,414,628,602.46, ikiwa ni asilimia 30.83, ambapo mnufaika mmoja mmoja ni sawa na asilimia 18.09,”alifafanua.
Badru aliongeza kuwa, fedha hizo zlizorejeshwa ni kutoka sekta ya elimu, ambazo ni asilimia 16.3, sawa na sh.12,440,208,125.47 na kwa upande wa huduma ni asilimia 12.09, sawa na sh.9,182,058,378.32.
“Katika mchanganuo huu, fedha zilizorejeshwa kutoka nyanja ya mawasiliano ni asilimia 5.47, sawa na shilingi 4,154,330,796.48, pia kwa upande wa sekta ya afya asilimia 1.05 sawa na shilingi 797,449,238.81,”aliongeza.
Alisema mchanganuo huo wa fedha unaonesha kuwa, fedha zilizorejeshwa kutoka sekta ya kilimo ni asilimia 0.89, sawa na sh.675,933,164.33 huku biashara ikilirejesha asilimia 2.34, sawa na sh. 1,777,172,589.35.
Mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya sekta zilizorejesha fedha hizo za mikopo kutoka migodini kuwa ni asilimi 0.88, sawa na sh. 668,338,409.67 huku gesi, mafuta na nishati ni asilimia 0.87, sawa na sh. 660,743,655.02.
“Kwa upande wa sekta ya ujenzi ni asilimia 0.62, sawa na shilingi 470,874,788.63, usafirishaji imerejesha shilingi 227,842,639.66, sawa na asilimia 0.30 na nyanja ya utalii asilimia 0.11, sawa na shilingi 83,542,301.21,” alifafanua Badru.
Mkurugezi mtendaji huyo alisema hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2016/2017, zaidi ya sh. 13,738,91,171.54, zilikuwa zimerejeshwa kwa mnufaika mmoja mmoja na kwamba, Juni, mwaka huu, wanufaika 139,259 walitambulika, ambapo kati ya hao, 45,590 walitambuliwa katika kipindi cha Julai hadi Juni, mwaka huu, ambapo wanadaiwa sh. 349, 970,196,982.38.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment