JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
limesema askari wake, Praiveti Mussa Jumanne, ambaye alikuwa katika
ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), amefariki.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa askari huyo
alifariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, askari huyo alipigwa
risasi na kundi la waasi nchini humo, katika tukio lililotokea Septemba 17,
mwaka huu.
Kufuatia shambulizi hilo, taarifa hiyo ilisema
Umoja wa Mataifa (UN), umeunda Bodi ya Uchunguzi kwa ajili ya kuchunguza tukio
hilo.
Aidha, maofisa na askari wa JWTZ, wanaendelea na majukumu yao katika operesheni hiyo DRC.
Imeongeza kuwa, Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu
wa kuuleta nchini mwili wa marehemu, ambapo taratibu za mapokezi, kuaga mwili
na mazishi zitatolewa baadaye.
No comments:
Post a Comment