SIKU chache baada ya mawaziri wawili katika Baraza la Mawaziri, lililoundwa na Rais Dk. John Magufuli, Desemba 10, mwaka juzi, kujiweka pembeni kutokana na kukabiliwa na tuhuma za biashara haramu ya madini ya tanzanite na almasi, baadhi ya mawaziri matumbo yameanza kupata joto.
Mawaziri hao matumbo yameanza kupata joto kutokana na wasiwasi walionao kuhusu nafasi zao, kwani wakati wowote Rais Magufuli atalazimika kulipangua baraza hilo ili kujaza nafasi zilizo wazi ama kuwaondoa mawaziri ambao ataona hawaendani na kasi yake ya 'Hapa Kazi Tu'.
Mawaziri wa mwisho kujiuzulu ni George Simbachawene, ambaye alikuwa katika Wizara ya
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Simbachawene na Ngonyani walimwandikia Rais Magufuli barua ya kuomba kujiuzulu katika nafasi zao mwishoni mwa wiki iliyopita, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kuhusu uchimbaji na uendeshaji wa biashara ya tanzanite na almasi.
Kujiuzulu kwa mawaziri hao kulitokana na agizo la Rais Magufuli, kuwataka wote walioguswa kwenye ripoti za kamati mbili za bunge, zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kujitafakari kwa kujiweka pembeni ili kupisha mamlaka zinazohusuka kuchunguza tuhuma zinazowakabili.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo Septemba 7, mwaka huu, baada ya kupokea ripoti hizo kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu, Dar es Salaam. Awali, Majaliwa alipokea ripoti hizo kutoka kwa Spika Ndugai, katika halfa iliyofanyika Septemba 6, mwaka huu, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Katika ripoti zake, kamati hizo mbili zilizokuwa chini ya wenyejiti Mussa Azzan Zungu (almasi) na Dotto Biteko (tanzanite), ziliitaka serikali iwachukulie hatua mawaziri watatu wa zamani wa wizara ya nishati na madini kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya madini hayo.
Mawaziri wa zamani waliotajwa kwenye ripoti hizo ni William Ngeleja, Sospeter Muhongo na George Simbachawene, ambao wanadaiwa kufanya makosa mbalimbali ya kiutendaji walipokuwa wakiiongoza wizara hiyo na kuisababishia serikali kupata hasara ya mamilioni ya fedha.
Mbali na mawaziri hao wa zamani, kamati hizo pia ziliitaka serikali iwachukulie hatua maofisa wa zamani wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), akiwemo Dk. Edwin Ngonyani, ambaye kabla ya kujiuzulu, alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano, wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo na mkurugenzi wa kitengo cha kuthaminisha madini.
Simbachawene na Ngonyani wamefanya idadi ya mawaziri waliolazimika kujiweka pembeni au uteuzi wao kutenguliwa na Rais Magufuli, wawe watano. Mwingine ni Charles Kitwanga, aliyekuwa akiiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa kutokana na tuhuma za kujibu maswali bungeni akiwa amelewa.
Wengine ni Nape Nnauye, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye aliwekwa pembeni kwa kushindwa kuisimamia vyema wizara hiyo katika sekta ya madini.
Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulimfanya Rais Magufuli amteue Dk. Harisson Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo huku nafasi ya Kitwanga ikichukuliwa na Mwigulu Nchemba, aliyehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Aidha, Rais Magufuli alimteua Profesa Paramaganda Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria ili kuchukua nafasi ya Dk. Mwakyembe. Hata hivyo, nafasi ya Profesa Muhongo hadi sasa iko wazi. Nafasi hiyo inashikiliwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.
Rais Magufuli pia alimbadili wizara, Profesa Makame Mbarawa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwenda Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano huku akimteua Injinia Gerson Lwenge kuchukua nafasi yake.
Nafasi zingine ambazo kwa sasa ziko wazi ni ya Simbachawene na Ngonyani, ambazo Rais Magufuli anaweza kuziziba kwa kuwabadili wizara baadhi ya mawaziri, ambao anawaona watafaa kuzishika.
Uteuzi pekee unaotajwa kuwa mgumu ni wa Wizara ya Nishati na Madini, ambayo mawaziri wake wa zamani wapo kikaangoni kutokana na kuruhusu kufanyika 'madudu' katika biashara ya tanzanite na almasi.
Wakati wa kupokea ripoti ya kamati alizoziunda kuchunguza uchimbaji na biashara ya madini, Spika wa Bunge, Ndugai aliishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuitenganisha
ili iweze kufanyakazi zake vizuri zaidi na kupunguza matatizo, ambayo yamekuwa yakijitokeza katika sekta ya madini.
Ndugai alisema kwa hali ilivyo sasa, wizara hiyo imekuwa ikikabiliwa na mzigo mkubwa wa kusimamia sekta hizo nyeti, hivyo kusababisha usimamizi mbovu, hasa katika sekta ya madini.
Mawaziri wengi kwa sasa wapo tumbo joto kuhofia kuteuliwa kuiongoza wizara hiyo nyeti, kutokana na uzito wa majukumu yake na pia mawaziri wengi wa zamani kukumbwa na kashfa mbalimbali.
Iwapo Rais Magufuli atatekeleza ushauri wa Spika Ndugai na wabunge wengine, huenda akaitenganisha wizara hiyo na kuzifanya ziwe mbili ama kuziunganisha na wizara zingine, jambo ambalo huenda likasababisha kazi iwe ngumu zaidi.
Mawaziri wa mwanzo kuteuliwa na Rais Magufuli katika baraza lake la mawaziri ni
Simbachawene na Angella Kairuki (Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora) na Suleiman Jafo (naibu).
Wengine ni January Makamba (Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira) na naibu wake Luhaga Mpina, Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu) akisaidiwa na Dk. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Mwigulu Nchemba (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), akisaidiwa na William Ole Nasha,
Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), akisaidiwa na Edwin Ngonyani, Philip Mpango (Wizara ya Fedha), akisaidiwa na Dk. Ashantu Kijaji, Profesa Mugongo (Nishani na Madini) akisaidiwa na Dk. Kalemani, Dk. Mwakyembe
(Katiba na Sheria).
Dk. Augustine Mahiga (Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki), akisaidiwa na
Dk. Susan Kolimba, Dk. Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Kitwanga (Mambo ya Ndani), William Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), akisaidiwa na Angelina Mabula, Profesa Jumanne Maghembe (Maliasili na Utalii), akisaidiwa na Ramo Makani; Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwekezaji); Profesa Ndalichako (Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi), akisaidiwa na Injinia Stella Manyanya; Ummy Mwalimu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), akisaidiwa na
Dk. Hamis Kigwangala.
Mawaziri wengine ni Nape (Habari, Utamaduni, Samaa na Michezo), akisaidiwa na Anastazia Wambura; Profesa Makame Mbarawa (Maji na Umwagiliaji), akisaidiwa na Isack Kamwelwe.

No comments:
Post a Comment