Wednesday 25 November 2015

MAJALIWA ATEMA CHECHE



WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Wizara ya TAMISEMI kueleza sababu za mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, (DART) kuchelewa.

Aidha ameagiza kukutana viongozi wa mradi huo leo ili kupata maelezo ya kina.

Majaliwa (pichani) aliyasema hayo jana Dar es Salaam, mara baada ya kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Ofi si ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kutoka kwa Katibu Mkuu wa ofi si wa wizara hiyo Jumanne Sagini.

Alisema hakuna sababu za msingi za kucheleweshwa kwa mradi huo ambao ulifi kia hatua za mwisho za utekelezaji hivyo atakapokutana na uongozi wa DART atataka majibu ya kina ni nini kimekwamisha mradi huo.

“Kama kuna taasisi za umma zinakwamisha mradi huo au kuna sababu za kina wazitaje ni zipi ili utekelezaji uweze kufanyika mara moja na wananchi waweze kupata huduma stahiki,” alisema.

Majaliwa pia amewataka wakurugenzi wa TAMISEMI na wakuu wa taasisi kuhakikisha wanapata nakala ya hotuba ya Rais Dk. John Magufuli ya kuzindua Bunge ili kufuata mwelekeo wa utendaji kazi wa serikali katika kufi kia maendeleo.

Alisema serikali inahitaji kuona mabadiliko ya utendaji kazi serikalini katika kipindi kifupi hivyo, kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa na watendaji na wataalamu wanapaswa kutumia elimu waliyonayo kwa ufanisi na ujuzi.

“Kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano,”alisema.

Aliongeza kuwa: “Ninyi wakurugenzi siyo desk offi cers bali ni fi eld offi cers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisema.

Alisema ni muhimu kuhimiza watendaji waliopo chini kuzingatia muda wa kufi ka kazini, muda wa kukaa kazini na kudhibiti muda wa kutoka kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana na kufi kia mipango na malengo ya kazi kwa siku.

Alisema watahakikisha wanajua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia kazini. Kwa upande wake, Katibu Mkuu Sagidi, alisema utekelezaji wa mradi wa DART umefi kia hatua ya kukamilika kwa miundombinu iliyojengwa na katika awamu ya kwanza na barabara maalum za mabasi makubwa zenye jumla ya urefu wa kilomita 21, karakana mbili za mabasi, vituo vidogo 27 vilivyojengwa katikati ya barabara vipo tayari.

Sagidi pia aliwataka watumishi wa Ofi si ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuepuka ubadhilifu wa fedha za umma.

Aidha wafanyakazi hao wamesisitizwa kusimamia kasi ya serikali katika utendaji kazi na kuepuka migogoro kwa jamii wanayoitumikia.

Alisema watendaji wa wizara hiyo wahakikishe wanasimamia kazi za serikali ikiwemo kuondokana na kero zinazowakabili wananchi.

Watumishi hao wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma, kuwahi kazini  pamoja na kujiepusha na ubadhirifu wa fedha za umma.

Alisema kufanya kazi kwa kujituma na kuwa waaminifu kwa wananchi ili kufi kia lengo la serikali la kuondoa matatizo yasiyo ya lazima kwa wananchi na kuwa historia.

Pia alisema malalamiko yatokanayo na ukosefu wa madawati katika sekta ya elimu ni muhimu mkuu wa shule kujua majukumu yake kwa kutoa taarifa kwa wizara husika ili kuboresha sekta hiyo.

Alisema pamoja na kazi nyingine kesho watakagua usafi katika sekta mbalimbali za manispaa ya jiji ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na ya milipuko yatokanayo na uchafu

No comments:

Post a Comment