Thursday 23 February 2017

JK AKUTANA NA RAIS WA CHAD NA MWENYEKITI MPYA WA KAMISHENI YA UMOJA WA MATAIFA

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete  akipokelewa na Rais wa Chad Idrissa Deby Atno. Kulia ni Waziri wa Elimu wa Chad.  Ahmat Ghazali Acyl.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimkabidhi Mwenyekiti Mpya wa AU,  Moussa Fakhi Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Chad  Idrissa Deby Itno Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu.
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  na mwenyeji wake  Moussa Fakhi, Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni ya AU katika mazungumzo ya pamoja kuhusu Kamisheni ya Elimu na Libya.
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu akipokelewa na mwenyeji wake  Mhe. Moussa Fakhi, Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nyumbani kwake N'Djamena

Na Mwandishi Maalum


Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20 Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Chad, Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad. 


Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Chad, Ahmat Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha, Diguimbaye Christian.

Ziara hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Deby wamezungumzia janga kubwa linaloinyemelea dunia na hasa nchi za uchumi wa kati na chini ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. 


Viongozi hao wamezungumzia haja ya nchi za bara la Afrika kuchukua hatua z amakusudi kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika nchi zao ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.

Azma hiyo inatokana na stadi kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma kielimu kwa miaka 50 hadi 70. 


Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka 2050, kazi na ajira takribani bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na maendeleo na matumizi ya teknolojia (automation).

Rais Deby amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. 


Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.

Mbali na mkutano wake na Rais wa Chad, Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Fakhi nyumbani kwake N'Djamena. 


Rais Mstaafu amempongeza Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. 

Viongozi hao wawili wamekuwa pia na mazungumzo yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu barani Afrika na masuala ya hali ya usalama ya Libya.

No comments:

Post a Comment