Thursday 16 February 2017

MASOGANGE NAYE ANG'ANG'ANIWA NA POLISI





MWANAMITINDO maarufu nchini, Agness Masogange, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii waliotakiwa kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Taarifa za kuaminika kutoka kituoni hapo jana zilieleza kuwa, Masogange aliamua kujisalimisha baada ya kupokea wito kutoka kituo hicho uliotolewa kwa wasanii mbalimbali maarufu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, msanii huyo aliwasili kituoni hapo saa tatu asubuhi na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Jina la msanii huyo lilitajwa na baadhi ya wabunge katika kikao chake cha 11, kilichomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, ambao walihoji kwa nini hakuwemo kwenye orodha ya majina yaliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Wasanii waliotajwa katika awamu ya kwanza ni Wema Sepetu, Petit Man, Khalid Mohamed (TID) na Tunda.

 

No comments:

Post a Comment